kcselogo
spacer
 
PRIMARY LEVEL
English Language Papers
Writing Compositions
Lugha ya Kiswahili Papers
Uandishi wa Insha
Mathematics Past Papers
Science Past Papers
Social & Religion Papers
Ecede Resources

 

SECONDARY LEVEL
Agriculture Past Papers
Arabic Past Papers
Art Design Past Papers
Aviation Past Papers
Biology Past Papers
Building Construction Papers
Business Studies Papers
Chemistry Past Papers
Computer Studies Papers
CRE Past Papers
Drawing Design Papers
Electricity Past Papers
English Language Papers
French Past Papers
Geography Past Papers
German Past Papers
Hindu Past Papers
History Past Papers
Homescience Papers
IRE Past Papers
Lugha ya Kiswahili Papers
Mathematics Past Papers
Metalwork Past Papers
Music Past Papers
Physical Education Papers
Physics Past Papers
Power Mechanics Papers
Woodwork Papers Papers
Other Disciplines
 

Kiswahili Notes

Katika somo hili la matamshi, tutashughulikia vitate na vitanza ndimi.Vitate ni maneno yanayotatiza kimatamshi.Utatanishi huu unatokana na; kukaribiana kimatamshi kwa sauti fulani.Mfano. posa poza.Mtamkaji
kuathiriwa na lugha ya kwanza au lugha nyingine;Mfano. mahali /mahari

Vitate

Vitanza ndimi

Sikiliza vitanza ndimi vifuatavyo kisha uvitamke.

Sitasitasita kusisitiza kuwa sita na sita si sita.
Vazi alilovua alivaa baada ya kulifua likamfaa sana.
Makoti Alikoti alipohukumiwa, alipiga magoti na kulivua koti kortini.
Juzijuzi mjuzi jasusi alikutana na mjusi akienda kumuona mchuuzi
akichuuza mchuzi.

Himizo

Muundo ni sura au namna kitu kinavyoonekana kwa nje .Soma mahojiano
yafuatayo kati ya mwandishi wa habari na mwanariadha huku ukizingatia
muundo wa mahojiano yenyewe.

Mwandishi: Hujambo dada?
Mwanariadha: Sijambo.
Mwandishi: Mimi ni Philip Okelo mwanahabari wa Shirika
Utangazaji la Mambo Leo.Ningependa
Utangazaji la Mambo Leo.Ningependaa
kukuhoji kuhusu kukuhoji kuhusu la ushindi
wako.Waeleze wasikilizaji majina yako.
Mwanariadha: Jina langu ni Janet Jelimo. Kwa jina la utani
naitwa Risasi.
Mwandishi: Kwa nini wanakuita Risasi?
Mwanariadha: Kwa sababu ya kasi yangu katika mbio.
Mwandishi: Hongera kwa kushinda medali ya dhahabu
katika michezo ya Olimpiki.
Mwanariadha: Asante!
Mwandishi: Je, mipango yako ya siku za usoni ni ipi?

Mwanariadha: Ningependa kupata medali nyingi zaidi za dhahabu na kuvunja
rekodi nyingi zaidi kabla ya kustaafu.
Mwandishi: Mbali na riadha, unashiriki mambo yepi mengine?
Mwanariadha: Tayari nimejiunga na Chuo Kikuu cha Fujihama ili
kujiendeleza kielimu.
Mwandishi: Unasomea nini?
Mwanariadha: Nasomea Uhandisi wa Tarakalishi.
Mwandishi: Una ujumbe gani kwa vijana?
Mwanariadha: Ningependa kuwahimiza vijana wajitolee na kukuza vipawa
vyao. Kila mtu amebarikiwa na kipawa fulani. Lakini watu wengi hupuuza
vipawa vyao na kukosa kuvikuza. Ni muhimu vijana kujipa muda na kutambua
vipawa walivyo navyo. Baada ya kuvitambua, wapaswa kujitolea na kutia
bidii ili waweze kunufaika kutokana na vipawa hivyo.

mu wa nyimbo hutokana na ujumbe uliomo katika wimbo wenyewe.
Endelea kufanya utafiti zaidi kuhusu nyimbo.
Ni nyimbo ambazo huimbwa na mlezi wa mtoto kwa sauti nyororo na mahadhi
taratibu ili kumtuliza mtoto,kumwongoa au kumfanya alale.

Sarufi ya lugha huwa uwanja mpana ambao unashirikisha mada kama vile aina
za maneno katika lugha na matumizi yake kisahihi na kimaana kwa kufuata
utaratibu uliokubalika na wanajamii wa lugha husika. Hali kadhalika,
huhusisha uakifishaji.
Somo hili linahusisha ufundishaji wa kila aina ya maneno katika lugha na
matumizi ya maneno hayo kisahihi, kimaana na kisarufi. Somo hili
litakuwezesha kukuza kiwango chako cha msamiati na matumizi ya istilahi
mbalimbali.

Sarufi na matumizi ya lugha hushirikisha shughuli za kimawasiliano na
kimaingiliano kwa sababu mbalimbali katika miktadha tofauti tofauti na
mazingira halisi. Ufunzaji na ujifunzaji wa sarufi na matumizi ya lugha
humpa mwanafunzi nyenzo za kuwasiliana kikamilifu.

Mwandishi: Asante kwa kutembelea Idhaa hii. Vijana wamepata kujifunza
mengi kutoka kwako. Tunakutakia kila la heri.
Mwanariadha: Asante sana.

Tanbihi

Inadhihirika kuwa mahojiano huwa na maswali elekezi ya kudadisi undani wa
jambo fulani.
Mahojiano yanaweza yakashirikisha mada mbalimbali kutegemea muktadha.
Mahojiano yanaweza yakashirikisha mada mbalimbali kutegemea muktadha.
Shughuli
Kufikia mwisho wa kipindi hiki, unatakiwa uwe na uwezo wa:
i) kueleza maana ya mazungumzo
ii) kutambua muundo na sifa za mazungumzo
iii) kubainisha miktadha mbalimbali ya mazungumzo
iv) kutambua umuhimu wa mazungumzo

Tazama na kusikiliza mazungumzo A na B katika video hii. Tambua matukio
yote katika shughuli hizi mbili.

Video A Marafiki wawili wamekutana mtaani baada ya muda mrefu. Haya ni
mazungumzo ya kirafiki kuhusu maisha yao ya hapo awali na ambavyo
yameendelea.
Video B Kuna mazungumzo kati ya wakulima wawili wanaokutana katika kituo
cha malipo. Wanazungumza juu ya mavuno haba na malipo duni waliyopata
kutokana na hali mbaya ya anga.

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.
(Mwalimu na mwanafunzi wako nje ya sebule ya walimu)
Mwanafunzi: Shikamoo mwalimu.
Mwalimu : Marahaba! U hali gani ?
Mwanafunzi: Sina neno mwalimu ila ningependa kuomba msaada wako kuhusu
hotuba na mazungumzo.
Mwalimu : Shida yenyewe ni ipi?
Mwanafunzi: Aaa;Aa;nimeshindwa kubaini tofauti kati ya vipengele hivi
viwili.
Mwalimu : (Akionyesha kushangaa) Lo! Kwani jana hukuwepo darasani
tukijadili mambo haya?
Mwanafunzi: Samahani mwalimu nilikuwa hospitalini kwa matibabu.
Mwalimu : Pole, Utapata nafuu.
Mwanafunzi : Ahsante, nishapoa.

Mwalimu : Tofauti kuu kati ya hotuba na mazungumzo ni kwamba hotuba
huwasilishwa na mtu mmoja kwa hadhira fulani nayo mazungumzo ni maongezi
kati ya watu wawili au zaidi. Hotuba huchukua umbo la maelezo kuhusu
jambo fulani ilhali mazungumzo huchukua umbo la kitamthilia.
Mwanafunzi : Ahsante mwalimu, kunazo tofauti zingine?
Mwalimu : Ndiyo, lugha inayotumiwa katika hotuba huwa na urasmi fulani,
mazungumzo hutegemea muktadha. Lugha inayotumika hotelini haina urasmi
ilhali ile itumikayo ofisini huwa na urasimu. mazungumzo katika
hoteli,hospitali,kituo cha polisi na kadhalika. Mwanafunzi :
(Anatabasamu) Nashukuru sana Mwalimu. Hakika umenitoa gizani.
Mwalimu : Karibu. Nenda darasani udurusu zaidi.

SIFA ZA MAZUNGUMZO

Nyimbo
Wimbo ni utungo ulioundwa kwa maneno au sauti zilizoteuliwa kisanii na
zenye utaratibu wa kimuziki.Sauti hizo hupanda na kushuka na kuibusha
hisia fulani kwa mwimbaji na msikilizaji. Nyimbo hazizingatii kaida zote
za ushairi kama ilivyo katika mashairi halisi.
 

WIMBO WA TAIFA

Umesikia na kuona nini ?
Huu ni wimbo wa Taifa la Kenya, unaoimbwa katika shughuli rasmi za
kitaifa kama vile :
-katika sherehe na shughuli za kitaifa na kimataifa
-wakati wa kupandisha bendera katika shule, vyuo na taasisi mbalimbali

umuhimu wa wimbo wa taifa la Kenya
hutambulisha taifa letu
huibua hisia za uzalendo
hukuza umoja
hukuza na kuendeleza utamaduni
ni ombi kwa Maulana
hufunza maadili
huzindua wananchi

KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA

Kusikiliza na kuzungumza ni stadi zinazoshirikisha shughuli za
kimawasiliano na kimaingiliano kwa sababu mbalimbali katika miktadha
tofauti tofauti na mazingira halisi.Katika kusikiliza na kuzungumza,
matamshi yafaayo ni muhimu.
Ufunzaji na ujifunzaji wa stadi hizi humpa mwanafunzi nyenzo za
kuwasiliana, kuingiliana na kutagusana ili kutimiza mahitaji mbalimbali.

Kwa mfano:

  1. Kujuliana hali
  2. Kupasha ujumbe
  3. Kuelimisha
  4. Kuelekeza
  5. Kuzindua/Kuhamasisha

Kuonya/kutahadharisha

7. Kuhimiza/kushawishi

8. Kuliwaza

9. Kutatua mizozo katika jamii

10. Kutumbuiza

Hitimisho Imetambulika wazi kuwa stadi ya kusikiliza na kuzungumza
itakufaa sana maishani!

UTANGULIZI

Katika somo hili la matamshi, tutashughulikia vitate na vitanza
ndimi.Vitate ni maneno yanayotatiza kimatamshi.Utatanishi huu unatokana
na;

* kukaribiana kimatamshi kwa sauti fulani.Mfano. posa ?poza.
* Mtamkaji kuathiriwa na lugha ya kwanza au lugha nyingine;Mfano.
mahali /mahari

 

  KCSE ONLINE Resources

 

Chat on facebook

Follow on twitter